Daniel's Homepage

Member Info


Journal Category

Journal Archive

Site Feed

Journal

Thursday,Oct 19 2006, 02:07:40 PM Machifu

Sijuwi tuanzie wapi ndugu zangu ili mpate kutuelewa

Walikuwa ni machifu wetu wa Tanganyika, heshima.

Wakiongozwa na simba wa nyika, heshima.

chifu Kinjeketile Ngwale mwana wa rufiji, yeye yeye

muanzishaji wa vita vya maji maji , uuhh,

na aliyetaka risasi kuzigeuza maji, heey


ni pale, waliponyanyaswa na kutweswa tena zion

jamani, waliingiwa na ile roho ya lion

e e eee wakatangaza vita na mababilon


wasukuma kwenye pamba walianzisha mgogoro , oohooo

wakiongozwa na chifu Makongoro

wachagga wao waliibuka kwenye mikahawa na kuwafanyia kweli , we

walikuwa na machifu Sina na mangi Meli

wangoni waliwapiga na wakaiteka peramiho bila huruma, yeah

pamoja na machifu Songea na Chabruma

kwa wamachinga mababilon waliingia na kutaka kujichanganya, waliumia

wakakumbana na chifu wao Makunganya,


ni pale, waliponyanyaswa na kutweswa tena zion

jamani, waliingiwa na ile roho ya lion

e e eee wakatangaza vita na mababilon


waliingia musoma na kukuta watu wamekwisha waona na kuwasoma

na kwa wakerewe wakakutana na chifu Lukonge, loh

wataalamu wanasema mganga akipata dawa wanga wanapagawa

wakaamua kuikimbia Mara maana ilikuwa imaraaa

kwa wahehe hata wale waliovaa kitasha waliuliwa,

waliongozwa pomaja na chifu Mkwawa, sawsawa

wazaramo wao walishajua kuwa mababilon wana hila,

mapema waliwatandika wakiwa pamoja na chifu wao Kibasila , tunakwambia


ni pale, waliponyanyaswa na kutweswa tena zion

jamani, waliingiwa na ile roho ya lion

e e eee wakatangaza vita na mababilon


wafipa nao hawakukaa peke yao bali waliwasaida wenzao,

na chifu Kimalaunga akiwa pamoja nao.

wayao nao kitambo walishakaa chemba pamoja na chifu wao Machemba

wanyamwezi pamoja na chifu Isike ,

wapogoro na wandengereko nao pia walikuwepo, uwoo

mababilon cha moto walikiona toka kwa machifu wetu

na huo ndio ulikuwa mwanzo wa heshima kwetu uuuooo Jah


ni pale, waliponyanyaswa na kutweswa tena zion

jamani, waliingiwa na ile roho ya lion

e e eee wakatangaza vita na mababilon

93 Views | Post Comments | Share with Friends

toggle3Guestbook

Post Comment
Subject:
Comments: